Watu wawili wauawa kwenye shambulizi la mabomu nchini Somalia
2021-11-12 09:17:56| cri

 

 

Raia wawili wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa jana kwenye shambulizi la mabomu yaliyotegwa ndani ya gari katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Ofisa mmoja wa polisi wa Somalia amesema, gari hilo lililokuwa na mabomu lililipuliwa karibu na msafara wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kwenye makutano ya Banadir mjini Mogadishu.

Hakuna kundi lolote linalotangaza kuwajibika na shambulizi hilo, lakini wapiganaji wa kundi la al-Shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi kama hayo mara kwa mara.