Serikali ya Ethiopia yaeleza kuunga mkono suluhisho la Kiafrika huku vurugu zikiendelea nchini humo
2021-11-12 09:20:49| CRI

Serikali ya Ethiopia imesema inaunga mkono suluhisho linaloongozwa na Afrika, huku vurugu zikiendelea katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, Dina Mufti, alipokutana na wanahabari, huku akisisitiza kuwa, ni matakwa ya serikali ya Ethiopia kukabiliana na matatizo kwa njia ya amani.

Amesema nchi hiyo daima inapendelea suluhisho la amani la migogoro, lakini kuna masharti ya kuzingatiwa ili kutimiza amani, na moja ya masharti hayo, ni kutambua serikali halali ya Ethiopia, iliyochaguliwa na Waethiopia wenyewe.