Watu wasiopungua 20 wauawa kwenye shambulizi kaskazini mwa Burkina Faso
2021-11-15 09:06:50| CRI

Waziri wa Usalama wa Burkina Faso Bw. Maxim Kone ametangaza kuwa watu wasiopungua 20 wakiwemo polisi 19 wameuawa jana kwenye shambulizi la kigaidi dhidi ya kikosi cha polisi wa Inata lililotokea mkoani Soum kwenye eneo la Sahel.

Amesema opresheni zinaendelea kufanyika. Wakazi wa huko wametakiwa kuwa macho na kushirikiana kikamilifu na jeshi.