Mjumbe wa AU atumai mgogoro wa Ethiopia utapatiwa ufumbuzi wa amani
2021-11-15 09:08:09| CRI

Mjumbe wa AU atumai mgogoro wa Ethiopia utapatiwa ufumbuzi wa amani_fororder_33

Mwakilishi wa juu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika katika pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo amesema ni matumaini yake kwamba migogoro inayoongezeka Kaskazini mwa Ethiopia itatuliwa kwa amani.

Kwenye taarifa yake, Obasanjo ambaye anakutana na watendaji wa Ethiopia amesema wahusika wa pande mbalimbali aliokutana nao wameeleza matarajio yao ya amani, usalama, na utulivu nchini Ethiopia, akisisitiza kwamba hakuna ufumbuzi wa kijeshi yakiwemo mapambano ya vita ambao utahakikisha utulivu wa kisiasa nchini, hivyo amewataka viongozi wa pande zote kusitisha mashambulizi yao ya kijeshi.

Kwa mujibu wa Obasanjo sababu kuu ya tofauti kati ya wahusika wa pande zote za mgogoro ipo kwenye njia ya kufikia mafanikio ya mwisho.