Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan laahidi kuunda serikali ya kiraia
2021-11-15 09:11:40| CRI

Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan laahidi kuunda serikali ya kiraia_fororder_44

Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan limeahidi kuwa litaunda serikali ya kiraia katika siku chache zijazo.

Kamati Kuu ya Madaktari ya Sudan imethibitisha kuwa msichana alifariki dunia kufuatia majeraha mabaya aliyoyapata kichwani kwenye maandamano yaliyofanyika tarehe 13 mjini Khartoum, ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 7. Tokea tarehe 25, Oktoba hali ya kisiasa ilipoanza kubadilika, raia 22 wamefariki dunia.

Habari nyingine kutoka kituo cha televisheni cha al Jazeera cha Qatar zinasema, vikosi vya usalama vya Sudan usiku wa tarehe 13 viliingia kwenye nyumba ya msimamizi wa makao makuu ya wanahabari ya kituo hicho mjini Khartoum na kumkamata bila kutangaza sababu.