Huenda Sudan Kusini isifikie lengo la chanjo ya COVID-19 kutokana na ukosefu wa usalama na mafuriko
2021-11-16 09:40:07| CRI

Huenda Sudan Kusini isifikie lengo la kuchanja angalau watu milioni 2.5 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2021 kutokana na ukosefu wa usalama na mafuriko katika maeneo ya vijijini.

Tangu ianze kutoa chanjo ya COVID-19 mnamo mwezi Aprili, Wizara ya Afya imeshachanja dozi kamili watu 92,276.

Meneja anayeshughulikia janga la COVID-19 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Sacha Bootsman amesema kwamba Sudan Kusini bado iko nyuma katika kufikia lengo la kuchanja asilimia 40 ya watu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Ameongeza kuwa bado wamekwama kusambaza dozi za chanjo ya Johnson&Johnson kwenye kaunti kutokana na mafuriko na ukosefu wa usalama nchini kote.