Umoja wa Mataifa watangaza uwepo wa dola za Marekani milioni 40 kwa ajili ya operesheni za dharura kaskazni mwa Ethiopia
2021-11-16 09:37:10| CRI

Umoja wa Mataifa watangaza uwepo wa dola za Marekani milioni 40 kwa ajili ya operesheni za dharura kaskazni mwa Ethiopia_fororder_埃塞

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa dola milioni 40 za Marekani tayari zipo kwa ajili ya kuongeza operesheni za dharura kwenye eneo lililoathiriwa na mgogoro la kaskazini mwa Ethiopia.

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia misaada ya dharura Martin Griffiths, amesema mamilioni ya watu huko kaskazini mwa Ethiopia sasa wanaishi kwenye mazingira ya hatari wakati ambapo msukosuko wa kibinadamu unaendelea kukua zaidi.

Baada ya kurejea kutoka Ethiopia, naibu katibu mkuu huyo anayeshughulikia masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya dharura amesema mahitaji yanazidi kuongezeka nchini humo, na kwamba fedha hizo zitasaidia mashirika ya misaada kufikia baadhi ya watu walio kwenye hatari zaidi.