Mkuu wa jeshi la Sudan asisitiza kuwa jeshi halina nia ya kuendelea na madaraka
2021-11-17 10:25:13| CRI

Mkuu wa jeshi la Sudan asisitiza kuwa jeshi halina nia ya kuendelea na madaraka_fororder_苏丹

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan na Kamanda Mkuu wa Jeshi Abdel Fattah Al-Burhan amerejea tena kauli yake kwamba jeshi halina nia ya kuendelea na madaraka.

Al-Burhan alitoa kauli hiyo Jumanne wakati akimpokea Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Molly Phee mjini Khatoum. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baraza hilo, kamanda mkuu wa jeshi amesisitiza utayari na uwazi wa jeshi wa kufanya mazungumzo yasiyo na masharti ambayo yatapelekea kufikiwa kwa utulivu na maendeleo nchini. Ametilia mkazo zaidi kufuata waraka wa katiba na kufanya mazungumzo ya kina na pande zote za kisiasa ili kukamilisha muundo wa mamlaka ya mpito na kufanya mpito wa kidemokrasia nchini humo kufanikiwa hadi utakapofanyika uchaguzi huru na wa haki Julai 2023.

Mbali na hayo ameahidi kuwaachia huru wanasiasa wanaoshikiliwa, isipokuwa wale watakaothibitishwa kufanya makosa ya jinai.