Maafisa 7 wa gereza nchini Kenya wakamatwa kwa kutoroka kwa wafungwa wa kigaidi
2021-11-17 10:27:33| CRI

Kenya imewakamata wasimamizi saba wa gereza kutokana na kutoroka kwa wafungwa watatu waliokuwa wakitumikia kifungo kwa makosa yanayohusiana na ugaidi.

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya Bw. Fred Matiangi amesema kwamba uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa sababu ya kutoroka katika gereza lenye ulinzi mkali ni ulegevu na uzembe.

Taarifa iliyotolewa na wiraza hiyo imesema kuwa hawataangalia upande wa uchunguzi tu bali pia watachukua hatua madhubuti ili kuhakikisha uzembe wa aina hii hautokei tena kwani unahatarisha maisha ya wananchi.

Ameongeza kuwa wamejiandaa vyema na wametuma ujumbe nchini kote, ambapo watafanya msako mkali wa kuwatafuta watatu hao.

Afisa huyo wa Kenya aliwataka Wakenya wasiwe na hofu kuhusu tukio hilo, akisema vikosi vya usalama viko katika hali ya tahadhari.