Kenya yaimarisha usalama baada ya kutokea kwa milipuko nchini Uganda
2021-11-17 10:21:35| CRI

Kenya yaimarisha usalama baada ya kutokea kwa milipuko nchini Uganda_fororder_头条乌干达

Kenya imeimarisha usalama na kuchukua tahadhari zaidi baada ya kutokea kwa milipuko miwili nchini Uganda ambayo imesababisha vifo vya watu 6 wakiwemo washambuliaji watatu waliojitoa mhanga, na wengine 33 kujeruhiwa.

Msemaji wa polisi ya Kenya Bw. Bruno Shioso amesema vikosi vya usalama vinaimarisha operesheni nchini kote pamoja na eneo la mpaka kati ya Kenya na Uganda, ili kuzuia shambulizi lolote la kigaidi.

Wakati huohuo Umoja wa Afrika umelaani milipuko hiyo iliyotokea Uganda na kusema uko pamoja na watu wa Uganda. Umoja huo pia umetoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia majeruhi wapone haraka.