TAZARA kuzindua mashindano ya gofu ili kuwaenzi viongozi waasisi wa Tanzania na Zambia
2021-11-17 10:26:44| CRI

Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ikishirikiana na Klabu ya Michezo ya Gymkhana ya Dar es salaama Tanzania inazindua mashindano ya mchezo wa gofu ili kuuenzi urafiki kati ya viongozi waasisi wa nchi mbili yaani hayati Julias Nyerere na mwenzake Keneth Kaunda, ambao ndio waliopanga kujengwa kwa reli hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TAZARA mashindano hayo ya gofu yatafanyika katika klabu ya Gymkhana ya Dar es salaama Disemba 9, 2021, ambayo pia ni siku ya Uhuru wa Tanzania na ni siku ambayo rais Kaunda alisafiri kutoka Zambia ili kusherehekea uhuru wa Tanzania kwa mchezo wa gofu mwaka 1987.

TAZARA ilijengwa kama mradi wa usafiri kati ya 1970 na 1975 kupitia mkopo usio na riba kutoka China, ambapo ilianza kufanya kazi kibiashara Julai 1976, ikiwa na umbali wa kilomita 1,860 kutoka Dar es salaama Tanzania hadi Kapiri Mposhi Zambia.