UNHCR: Wakimbizi zaidi ya 7,400 wapokea chanjo ya COVID-19 nchini Ethiopia
2021-11-18 09:28:19| CRI

Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema kuwa takriban wakimbizi 7,425 wanaoishi Ethiopia wamepokea chanjo ya COVID-19.

Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema kwamba takriban wakimbizi 4,481 wamechanjwa kikamilifu, ambao wanakidhi vigezo vya kipaumbele vya serikali.

Kulingana na takwimu kutoka UNHCR, Ethiopia ni nchi ya tatu kwa kuhifadhi wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, ambapo hadi kufikia Oktoba 2021 nchi hiyo imekuwa na wakimbizi 806,374 waliosajiliwa na wanaotafuta hifadhi, na wengi wao wanatoka Sudan Kusini, Somalia, Eritrea na Sudan.