Kenya yaanza mazungumzo ili kutimiza mpango wa utengezaji wa chanjo ya COVID-19 hadi kufikia 2024
2021-11-19 10:43:45| CRI

Kenya yaanza mazungumzo ili kutimiza mpango wa utengezaji wa chanjo ya COVID-19 hadi kufikia 2024_fororder_肯尼亚 头图

Kenya imeanza mazungumzo na nchi nyingine mbalimbali ili kutimiza mpango wa kuweka kiwanda cha kutengeza chanjo ya COVID-19 hadi kufikia 2024.

Katibu Mkuu Utawala wa Wizara ya Afya Rashid Aman amesema Kenya inawasiliana na nchi mbalimbali ili kupata utafiti, teknolojia, viungo vya dawa na kuunga mkono uzalishaji wa bidhaa nyingine za huduma za afya. Bw. Aman amesema upungufu wa chanjo ya COVID-19 ulioikumba dunia hivi karibuni umeihamasisha Kenya kujenga haraka kituo cha kutengeneza chanjo hiyo kiitwacho Kenya Biovax Limited. Nchi zinazotengeza chanjo ya COVID-19 duniani ni pamoja na China, Marekani na Russia, ambapo baadhi yake Kenya imepata chanjo yao.