Uzalishaji umeme wapungua Tanzania kwa 345MW kutokana na kupungua kwa viwango vya maji katika mito na mabwawa
2021-11-19 10:44:44| CRI

Uzalishaji umeme wapungua Tanzania kwa 345MW kutokana na kupungua kwa viwango vya maji katika mito na mabwawa_fororder_坦桑

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuwa kutakuwa na upungufu wa uzalishaji umeme unaotokana na kupungua kwa viwango vya maji katika mito na mabwawa.

Kwenye taarifa yake TANESCO limesema uzalishaji huo umepungua kwa takriban megawati 345, ambayo ni sawa na asilimia 21 ya uzalishaji wote. Hata hivyo taarifa hiyo haikutaja matumizi ya kila siku ya uzalishaji umeme lakini limehusisha upungufu huo unatokana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa mujibu wa taarifa, uzalishaji wa umeme umeathiri sana vituo vinavyozalisha umeme vya TANESCO vikiwemo Kihansi, Pangani na Kidatu.

TANESCO imesema inachukua hatua za haraka kuzalisha umeme kupitia vituo vyake vinavyotumia gesi asilia.