Huduma ya internet yarejea Sudan
2021-11-19 10:46:32| CRI

Shirika la habari la Sudan SUNA limesema huduma ya internet inarejea taratibu kupitia kampuni za mawasiliano nchini humo.

Huduma ya Internet ilisimamishwa tarehe 25, Oktoba baada ya kamanda mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan kuchukua hatua ikiwemo kuvunja Baraza la Mamlaka na serikali.

Tarehe 9, Novemba, mahakamaya Sudan ilitoa uamuzi wa kutaka kampuni za mawasiliano kurejesha mara moja huduma ya internet, lakini wakati huo mamlaka ya utawala haikutekeleza uamuzi huo.