Serikali ya Ethiopia yasema wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wataachiliwa ikiwa polisi hawana ushahidi
2021-11-19 10:45:49| CRI

Serikali ya Ethiopia imesema kwamba wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaozuiliwa kama sehemu ya hatua kubwa inayoendelea ya utekelezaji wa sheria nchini Ethiopia wataachiliwa ikiwa polisi hawatatoa ushahidi.

Kauli hiyo ilitolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Bw. Dina Mufti, huku akisisitiza kuwa ripoti za kuzuiliwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa hazina uhusiano wowote na shirika ambalo wanalifanyia kazi. Ameongeza kuwa inachofanya serikali ni kutekeleza sheria, hivyo ni wale tu wanaokiuka sheria na kanuni zilizopo nchini ndio wanaowajibika.

Bw. Mufti amesisitiza kuwa hakuna mtu atakayechunguzwa au kushikiliwa na mtu yeyote kwa sababu anatoka katika kabila fulani, nchi fulani au eneo fulani.