Waethiopia waishio nchi za nje wakusanyika kupinga uingiliaji wa nje kwenye mambo ya ndani ya nchi yao
2021-11-22 08:42:57| CRI

Waethiopia waishio katika miji ya New York, Washington, London, Toronto na Jerusalem jana Jumapili walikusanyika wakipinga uingiliaji wa nje kwenye mambo ya ndani ya nchi yao.

Maandamano hayo yenye kaulimbinu ya “No More” pia yameungwa mkono na watu wa nchi nyingine za Afrika wanaoishi katika nchi hizo, yanalenga kuonyesha msimamo wao kuzitaka baadhi ya nchi za magharibi kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya Ethiopia, na kutoa wito kwa vyombo vya habari vya kimataifa kuacha kusambaza taarifa potofu kuhusu Ethiopia.

Habari zinasema, maandamano hayo yataendelea katika miji mingine duniani.