Maonyesho ya biashara kati ya nchi za Afrika yafungwa kwa makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 36 kusainiwa
2021-11-22 09:31:56| CRI

Maonyesho ya biashara kati ya nchi za Afrika ya mwaka 2021 (IATF2021) yalimalizika jana huko Durban nchini Afrika Kusini, ambapo makubaliano ya biashara yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 36 yamesainiwa.

Mkurugenzi mkuu wa mpango wa biashara ya ndani ya Afrika wa Benki ya Exim ya Afrika Bibi Kanayo Awani alitangaza habari hiyo kwenye ufungaji wa maonesho hayo.

Bibi Awani amesema jumla ya watu 11,828 na makampuni 59 ambayo 46 kati ya hayo ni ya kutoka bara la Afrika, yalishiriki kwenye maonesho hayo.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la maonyesho hayo Bw. Olusegun Obasanjo amepongeza mafanikio yaliyopatikana kwenye maonyesho hayo, licha ya kuwepo kwa changamoto ya COVID-19.