Tanzania yawataka viongozi wanawake kuhimiza uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake
2021-11-22 09:02:02| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ameutaka mtandao wa viongozi wa wanawake wa Afrika (AWLN) kuendelea kutunga sera na sheria zitakazohimiza uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake.

Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, imesema Rais Samia ametoa mwito huo kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya video kujadili uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake kwenye maeneo mbalimbali ya maendeleo. Rais Samia amesema Tanzania imeanzisha mabaraza ya kuwawezesha wanawake kiuchumi katika nchi nzima.

Rais Samia pia amezungumzia maswala mengine yanayohusu Tanzania kama vile kuhimiza uwazi kwenye matumizi ya umma, kuimarisha mapambano dhidi ya COVID-19 na kusema serikali yake itaendelea kukabiliana na maswala yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, yaliyotokana na mvua chache na kuathiri uzalishaji wa kilimo.