Uchunguzi wa Afrobarometer waonesha China inaongoza kwa ushawishi barani Afrika
2021-11-23 08:21:08| CRI

Uchunguzi wa Afrobarometer waonesha China inaongoza kwa ushawishi barani Afrika_fororder_中非头图

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na shirika la uchunguzi wa maoni la Afrobarometer inaonesha kuwa China inaongoza kwa ushawishi barani Afrika. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian jana Jumapili alisema, kunufaishana ni msingi wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 63 ya wahojiwa wanaona China ina ushawishi mkubwa kisiasa na kiuchumi kwa nchi zao, asilimia 66 ya wahojiwa wanaona ushawishi wa China kisiasa na kiuchumi kwa nchi zao ni chanya.

Bw. Zhao Lijian amesema,kwa upande wa biashara, China imekuwa nchi kubwa ya kwanza ya biashara kwa Afrika kwa miaka 12 mfululizo, na kwa upande wa miundombinu, Afrika imekuwa soko kubwa la pili kwa wakandarasi wa miradi wa China. Amesisitiza kuwa China siku zote imekuwa ikishikilia kuendeleza ushirikiano na Afrika kwa kuzingatia maslahi na mahitaji yake na bila masharti ya kisiasa. China inapenda kutumia fursa ya mkutano wa FOCAC utakaofanyika mwaka huu nchini Senegal, kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika.