Ushirikiano kati ya China na Afrika waendelea kuimarika huku kukiwa na janga la COVID-19
2021-11-24 08:48:28| CRI

Ushirikiano kati ya China na Afrika waendelea kuimarika huku kukiwa na janga la COVID-19_fororder_VCG111164721339 (2)

Mawaziri wa nchi za Afrika na China watakutana mjini Dakar Senegal wiki ijayo kwa ajili ya mkutano wa nane wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC.

Mawaziri hao wanakutana wakati janga la COVID-19 bado linaendelea duniani na kuathiri uchumi wa nchi nyingi, hasa nchi za Afrika kusini mwa Sahara, na kurudisha nyuma baadhi ya mafanikio yaliyopatikana.

Akiongea na wanahabari mjini Kampala kuhusu mkutano huo utakaofanyika tarehe 29 na 30, Balozi wa China nchini Uganda Bw. Zhang Lizhong, amesema changamoto kama janga la COVID-19 imeleta majaribu kwenye uhusiano kati ya China na Afrika na kufanya uhusiano huo uzidi kuimarika.

Amesema mshikamano na ushirikiano ni silaha yenye nguvu ya kulishinda janga la COVID-19 na bila shaka mwanga wa ushirikiano utatokomeza janga hilo.

Mbali na mkutano wa mawaziri pia kutakuwa na mikutano mingine inayohusu sekta mbalimbali za ushirikiano.