Afrika Kusini na Kenya zakubaliana kuinua kiwango cha uhusiano
2021-11-24 14:25:37| cri

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana mjini Pretoria alikutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta, na kusema umefika wakati wa kuinua kiwango cha uhusiano kati ya nchi zao na kuwa wa “wenzi wa kimkakati”.

Viongozi hawa wawili walisisitiza umuhimu wa mkakati wa uhusiano kati ya nchi zao na kurejea ahadi ya kuinua kiwango cha uhusiano huo kupitia Makubaliano ya Wenzi wa Kimkakati.

Wakati nchi hizo zinapanga kukuza biashara na uwekezaji, rais Ramaphosa amesema hatua ya kuinua kiwango cha uhusiano inaweza kuwa muhimu kwa sekta nyingine.

Rais Kenyatta anatarajiwa kumaliza ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini  leo Jumatano.