Waziri mkuu Sudan ataka kuimarishwa usalama katika maandamano ya Alhamisi na kuachiwa kwa wanaoshikiliwa
2021-11-25 09:51:58| cri

Waziri mkuu Sudan ataka kuimarishwa usalama katika maandamano ya Alhamisi na kuachiwa kwa wanaoshikiliwa_fororder_苏丹

Waziri mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok ametaka usalama kuimarishwa wakati wa maandamano ya Alhamisi na kuanza mara moja mchakato wa kuwaachia huru watu wanaoshikiliwa.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema Bw. Hamdok alitoa amri hii alipokutana na viongozi wa polisi ya Sudan, ambao walipitia mpango kabambe wa kuhakikisha usalama wakati wa maandamano na kusisitiza haki ya kutoa maoni kwa njia ya amani kwa mujibu wa katiba na kanuni za Mapinduzi ya Sudan yaliyomwondoa madarakani rais wa zamani Omar al-Bashir mwaka 2019. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mchakato wa kuwaachia huru wanaoshikiliwa utafanyika kote nchini.

Mji mkuu Khartoum na miji mingine nchini Sudan leo alhamisi inatarajiwa kushuhudia maandamano yanayodai serikali ya kiraia.