Watu 43 wauawa, vijiji 46 vyachomwa moto na kuporwa katika jimbo la Darfur
2021-11-26 08:44:19| CRI

Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, imesema watu 43 wameuawa na vijiji 46 vimechomwa moto na kuporwa  katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Taarifa iliyotolewa na OCHA imesema mapambano yalitokea tarehe 17 kati ya wafugaji waarabu na wakulima wa kabila la Jebel Misseriya katika eneo la Jebel Moon. Mbali na taarifa za watu 43 kuuawa na vijiji 46 kuchomwa moto, idadi ya watu waliojeruhiwa kwenye mapambano hayo yanayoendelea bado haijulikani, lakini watu kadhaa ikiwa ni pamoja na watoto hawajulikani walipo.

Serikali ya mpito ya Sudan iliamua kukomesha mgogoro katika jimbo la Darfur kupitia makubaliano yaliyofikiwa Oktoba 3 mwaka jana, lakini baadhi ya makundi bado hayajasaini makubaliano hayo.