Wasomi wa nchi za Afrika wasema uzoefu wa China unastahili kuigwa ili kutafuta njia ya maendeleo inayofaa hali halisi ya nchi zao
2021-11-26 14:55:52| CRI

Wasomi wa nchi za Afrika wasema uzoefu wa China unastahili kuigwa ili kutafuta njia ya maendeleo inayofaa hali halisi ya nchi zao_fororder_VCG111164782654

Mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika kuanzia Novemba 29 hadi 30 mjini Dakar, Senegal. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mawaziri wa China na nchi za Afrika kukutana ana kwa ana tangu janga la virusi vya Corona lilipolipuka, na hivyo kufuatiliwa sana na jamii ya kimataifa.

Msomi kutoka Somalia na naibu mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Bi. Hodan Osman Abdi ameeleza matarajio yake kuwa FOCAC itatoa msukumo zaidi kwa maendeleo ya Somalia. Amesema, FOCAC siku zote ni jukwaa muhimu la kuunga mkono maendeleo ya Afrika. Amesema China ni nchi kubwa, na kutendewa kwa usawa na China kumeongeza kwa kiasi kikubwa imani ya nchi za Afrika kujiendeleza na kujitegemea. Bi. Hodan anatarajia kuwa mkutano wa Dakar utafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya Somalia na China. Amesema, Somalia ina hali nzuri kijiolojia, hifadhi kubwa ya malisili na idadi kubwa ya vijana, anatumai kuwa FOCAC itaunga mkono zaidi miradi inayohitajika sana ya maendeleo, ikiwemo miundombinu nchini Somalia, ili kuisaidia nchi yake kubadilisha raslimali ilizo nazo kuwa matokeo halisi ya maendeleo.

Naye mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa China ya Nigeria Bw. Onunaiju Charles Okechukwu anaona kuwa, kubadilishana uzoefu wa utawala wa nchi kunapaswa kuwa nyanja muhimu ya ushirikiano kati ya Afrika na China katika hatua zijazo. Ingawa haiwezekani kunakili wala kupandikiza mafanikio ya China katika nchi nyingine, lakini uzoefu wa China unastahili kuigwa. Amesema, kujifunza kutoka kwa China kunamaanisha kujifunza namna ya kutafuta njia ya maendeleo inayofaa hali halisi ya nchi husika, ili kuhamasisha kadri iwezekanavyo nguvu ya umma, na hivyo kutimiza maendeleo shirikishi na endelevu.