IGAD na EU zalaani shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu
2021-11-26 09:30:58| cri

Shirika la Maendeleo la Kiserikali za Nchi za Afrika Mashariki IGAD na Umoja wa Ulaya, wamelaani shambulizi la kujitoa muhanga kwa kutumia mabomu yaliyotegwa ndani ya gari lililotokea mapema Alhamisi mjini Mogadishu, na kusababisha vifo vya watu wanane na wengine 17 kujeruhiwa.

Polisi ya Somalia imesema shambulizi hilo la kigaidi lililodaiwa kufanywa na kundi la wapiganaji la al-Shabaab, lililenga msafara wa kampuni ya usalama inayotekeleza jukumu la kulinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. IGAD na Umoja wa Ulaya kila upande umetoa taarifa zikisema shambulizi hilo halitazuia juhudi za kusaidia na kutuliza hali ya Somalia.

Shambulizi hilo kubwa ambalo pia limeharibu majengo kadhaa limetokea wakati uchaguzi wa wabunge unaendelea nchini Somalia.