Uchumi wa Tanzania wakadiriwa kukua kwa asilimia 5 mwaka huu
2021-11-26 09:16:00| CRI

Gavana wa benki kuu ya Tanzania Bw. Florens Luoga katika ufunguzi wa mkutano wa 20 wa mashirika ya kifedha wa Tanzania uliofanyika huko Dodoma, amesema kuwa uchumi wa Tanzania kwa mwaka huu unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5, na unatarajiwa kukua kwa zaidi ya asilimia 8 katika miaka mitano ijayo.

Amesema makadirio hayo yanategemea ongezeko la matumizi ya raslimali na ongezeko la uzalishaji.

Mkutano huo wa siku mbili umewavutia zaidi ya wataalam 300 wa ndani na nchi za nje, wakiangalia upya jinsi Tanzania itakavyoweza kuhimiza ufufuaji wa uchumi na kuhakikisha ukuaji endelevu baada ya janga la COVID-19.