Upanuzi wa chuo VETA kwa msaada wa China nchini Rwanda wakamilika
2021-11-26 08:43:49| CRI

Upanuzi wa chuo VETA kwa msaada wa China nchini Rwanda wakamilika_fororder_卢旺达

Upanuzi wa Chuo cha VETA sehemu ya Musanze nchini Rwanda umekamilika baada ya ujenzi uliofanyika kwa miaka miwili na kukabidhiwa kwa Rwanda.

Upanuzi huo uliofanyika kwa msaada kutoka serikali ya China, ulihusu ujenzi wa ukumbi wa matumizi mbalimbali, jengo la utawala, jengo la madarasa, mabweni ya wanafunzi, karakana za mafunzo, eneo la michezo  na eneo la maegesho.

Sehemu ya kwanza ya ujenzi wa chuo hicho ilikamilika mwaka 2015 na kuwa chuo kikubwa zaidi cha VETA kinachomilikiwa na serikali katika mkoa wa kaskazini.

Waziri wa nchi wa Rwanda anayeshughulikia mambo ya Tehama na vyuo vya VETA Bibi Claudette Irene, ameishukuru China kwa msaada huo na kusema China kuipatia Rwanda msaada huo mkubwa ni alama ya urafiki mzuri uliopo kati ya China na Rwanda.