Tanzania yaonya uhaba wa maji na upungufu wa maeneo ya malisho ya wanyama
2021-11-29 08:15:18| CRI

Mamlaka nchini Tanzania jana imeonya kuwa kwamba, ukame wa muda mrefu katika maeneo mbalimbali ya nchi unaotokana na mabadiliko ya tabianchi umesababisha uhaba wa maji na kupungua kwa maeneo ya malisho ya mifugo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira, Seleman Jafo ameitaja mikoa mitatu nchini humo, Dar es Salaam, Dodoma na Morogoro, na kusema inakabiliwa na uhaba wa maji, na baadhi ya wanyama wamekufa kutokana na upungufu wa maeneo ya malisho na maji.

Waziri Jafo amesema hayo mjini Dar es Salaam baada ya mashindano ya kilomita 10 ya mbio za baiskeli yaliyoandalizwa na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania katika kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.