Ofisa wa AU yapongeza uhusiano wa kina wa China na Afrika
2021-11-29 08:23:54| CRI

Kamishna wa Afya, Masuala ya Kibinadamu na Maendeleo ya Jamii wa Umoja wa Afrika (AU) Amira Elfadil amepongeza uhusiano wa kina wa China na Afrika katika maeneo mbalimbali, hususan ushirikiano katika huduma za afya.

Bi. Elfadil amesema hayo alipohojiwa na Shirika la Habari la China, Xinhua, kabla ya mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaoanza leo mjini Dakar, Senegal. Ameishukuru serikali ya China kwa ushirikiano mzuri, pia amewashukuru wadau wote wanaofanya kazi kujenga uhusiano mzuri na wa nguvu zaidi kati ya China na Afrika, na kati ya China na Kamati za Umoja wa Afrika.

Kamishna huyo amepongeza uhusiano wa China na Afrika katika sekta ya afya, na kusema ni ushuhuda wa ushirikiano wa kunufaishana ambao unahitaji kuboreshwa zaidi.