Guinea-Bissau yajiunga kwenye Pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja
2021-11-29 08:52:22| cri

Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China imesema, balozi wa China nchini Guinea-Bissau Bw. Guo Ce na waziri wa mambo ya nje wa Guinea-Bissau Bi. Suzi Carla Barbosa, wamesaini makubaliano ya awali kuhusu Pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI), na kuifanya nchi hiyo kuwa mwanachama mpya wa Pendekezo hilo.

Hivi sasa, China imesaini makubaliano zaidi ya 200 ya ushirikiano wa BRI na nchi 142 na mashirika 32 ya kimataifa.