Thamthiliya na filamu za China zapendelewa na watazamaji wa Afrika
2021-11-29 10:42:01| CRI

Thamthiliya na filamu za China zapendelewa na watazamaji wa Afrika_fororder_微信图片_20211129092607

Hivi karibuni kampeni ya The Bond 2 imemalizika. Katika mwezi mmoja uliopita,tamthiliya,filamu na katuni zaidi ya 50 za China zilizotiwa sauti kwa lugha sita ikiwemo kiswahili,kihausa,kireno,kifaransa,kiarabu na kiingereza zimeoneshwa vyombo vikuu 20 vya habari barani Afrika.

“The Bond 2”ikiwa na kaulimbiu ya “Ushirikiano kati ya China na Afrika, maisha ya watu wa kawaida, kuondokana na umaskini na urithi wa utamaduni”, imeonesha filamu, tamthiliya na katuni bora za China zilizotengenezwa katika miaka ya hivi karibuni, ikiwemo filamu za makala za shirika la utangazaji la taifa la China kama vile “Miradi Mikuu” na “Kuondokana na Umaskini”.

Hadi kufikia tarehe 25, maonesho hayo ya filamu na tamthiliya hizi yamewafikia watazamaji takriban milioni 300, huku shughuli hiyo ikikusanya dodoso zaidi ya elfu 26 kutoka watumiaji wa mtandao wa Internet kutoka nchi 86 duniani.