FOCAC ni jukwaa thabiti la kukuza uhusiano kati ya China na Afrika
2021-11-29 09:03:54| CRI

FOCAC ni jukwaa thabiti la kukuza uhusiano kati ya China na Afrika_fororder_f636afc379310a551b0eaed3ba4543a9822610ea

Waziri wa Fedha wa Ethiopia Ahmed Shide amesema, Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ni jukwaa bora na thabiti la kukuza ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Shide amesema, katika miongo miwili iliyopita, FOCAC imethibitishwa kuwa jukwaa lenye ufanisi na nguvu katika kukuza ushirikiano kati ya Afrika na China, kwa kuhimiza maendeleo ya miundombinu barani Afrika, kukuza biashara, kuchochea uwekezaji wa moja kwa moja, kuanzisha mazingira bora ya kuhamasisha ujasiriamali, na kuleta ajira.

Shide amesema, kutokana na mfumo wa FOCAC, China imeisaidia Ethiopia kukamilisha miradi kadhaa mikubwa ya miundombinu, na imesaidia kuongeza ajira na kutokomeza umaskini. Ameongeza kuwa, Ethiopia na China zimedumisha urafiki mkubwa na kusaidiana wakati dunia inapokabiliwa na mabadiliko makubwa, pamoja na kupambana na janga la COVID-19.