Tanzania yaelekeza macho yake kwenye soko kubwa la maparachichi la China
2021-11-30 14:35:41| cri

Wadau wakubwa wa sekta ya kilimo cha bustani wameelekeza macho yao kwenye soko la maparachichi la China lenye thamanai ya dola milioni 133 za kimarekani, baada ya Afrika Kusini kuruhusu maparachichi ya Tanzania kufika kwenye soko lake.

Mkurugenzi Mkuu wa Taha Group Bi Jacqueline Mkindi amesema baada ya kufanikiwa kuingia kwenye soko la Afrika Kusini sasa wanajitahidi kushirikiana kwa karibu na serikali ya Tanzania kufuatilia na kujua utaratibu wa China ili kuweza kutoa njia ya wasafirishaji wa maparachichi wa Tanzania kufika kwenye soko lenye faida kubwa la China

Takwimu kutoka forodha za China zinaonesha kuwa kwa mwaka Beijing inahitaji tani 43,860 za maparachichi, zikiwa na thamani ya dola milioni 133.38 za Kimarekani. Ambapo hili ni soko kubwa kwa wazalishaji wa Tanzania.