Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Jamhuri ya Kongo
2021-11-30 08:39:57| CRI

Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi jana amekutana na waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Jamhuri ya Kongo Denis Christel Sassou Nguesso huko Dakar, Senegal, kabla ya ufunguzi wa mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

Wang Yi amesema, China inapenda kuimarisha uungaji mkono kati ya pande mbalimbali na ushirikiano wa kimkakati na kuhimiza ushirikiano wa sekta mbalimbali. Ameongeza kuwa, China inapenda kuwa mwenzi wa kuaminika wa Jamhuri ya Kongo katika maendeleo na ustawi, na kuunga mkono nchi hiyo kuimarisha uwezo wake wa kujiendeleza na kutimiza maendeleo anuwai.

Kwa upande wake, Christel amesema Jamhuri ya Kongo inapenda kuimarisha ushirikiano wa pande zote na China ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa, mchango wa China katika maendeleo ya Afrika unakubaliwa na pande mbalimbali, na Mkutano wa FOCAC utapata mafanikio na kuhimiza zaidi ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika.