Watu 11 wauawa katika shambulizi dhidi ya gereza nchini Nigeria
2021-11-30 08:32:32| cri

 

 

Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini Nigeria (NCoS) Bw. Francis Enobore jana amesema, watu 11 wameuawa na wafungwa 252 wametoroka kutoka gereza lililoko jimbo la Plateau nchini Nigeria, wakati kundi la watu wasiojulikana waliokuwa na silaha waliposhambulia gereza hilo Jumapili

Bw. Enobore alisema, mlinzi mmoja wa gereza hilo na wafungwa 9, pamoja na mtu mmoja mwenye silaha waliuawa kwenye shambulizi hilo.

Kulingana na msemaji huyo, baadhi ya washambuliaji na wafungwa 262 walitoroka kwenye ghasia, na hadi sasa wafungwa 10 wamekamatwa tena, na wengine 252 hawajapatikana.