Biashara kati ya China na Afrika yaongezeka kwa asilimia 27.4 katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka huu
2021-11-30 08:59:47| cri

Takwimu zilizotolewa na Idara ya Forodha ya China zimeonyesha kuwa, katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya jumla ya biashara ya bidhaa kati ya China na Afrika ilikuwa dola za kimarekani bilioni 209.8, ambayo imeongeza kwa asilimia 27.4 ikilingana na mwaka jana wakati kama huo.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, katika kipindi hicho, mauzo ya China barani Afrika yaliongeza kwa asilimia 24.5 na kufikia dola za kimarekani bilioni 122.5, na ongezeko la uagizaji bidhaa kutoka Afrika lilikuwa asilimia 31.7 na kufikia dola za kimarekani bilioni 87.4.

Idara hiyo imesema, Afrika Kusini, Nigeria, Angola, Misri na DRC ni washirika wakuu watano wa biashara wa China barani Afrika.