Waziri wa Ethiopia autaja ubalozi wa Marekani kama ‘ugaidi’
2021-11-30 14:35:17| cri

Waziri wa Ethiopia amefanya aangaliwe kwa jicho baya baada ya kuutaja Ubalozi wa Marekani nchini Ethiopia kama "gaidi anayepaswa kuondoka nchini humo”.

Bw. Eyob Takalign Tolina, Waziri wa fedha wa Ethiopia, ameutuhumu ubalozi wa Marekani uliopo mjini Addis Ababa kwa kuchochea ghasia na kuhimiza ugaidi. Kwenye post yake ya Facebook, amedai kwamba Ubalozi wa Marekani unachochea mivutano kwa kuleta hofu kupitia kutoa tahadhari za usalama.

Wiki iliyopita ubalozi ulionya kuhusu hatari ya shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Ethiopia na maeneo mengine nchini humo. Pia umewaonya raia wa Marekani kuondoka nchini humo kutokana na kuongezeka kwa ghasia wakati kundi la Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) likisonga mbele kuelekea Addis Ababa.