Uganda yasema operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya waasi wa ADF kuendelea
2021-12-01 08:44:17| CRI

Jeshi la Uganda limesema, operesheni yake ya pamoja ya kijeshi na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi ya waasi wa kundi la ADF itaendelea.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana mjini Kampala imesema, mashambulizi ya anga yaliyofanywa dhidi ya kambi za kundi hilo yalikuwa sahihi, na sasa wanaanza kufanya operesheni za ardhini kutafuta maficho ya waasi hao.

Taarifa hiyo imesema, shambulizi la anga lililofanywa jana asubuhi na jeshi hilo lililenga maeneo kadhaa ya kundi la ADF, ambalo linatuhumiwa kusababisha vurugu mashariki mwa DRC na kulipua mabomu katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.