Mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC wafungwa
2021-12-02 09:16:00| CRI

Mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC wafungwa_fororder_fb28f9594eb844189d5169308cc9d9c4

Mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika kuanzia tarehe 29 hadi 30 mwezi Novemba mjini Dakar, Senegal umefungwa, na wajumbe waliohudhuria mkutano huo wamefikia makualibano mengi.

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema mkutano huo umekumbusha maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika tangu kufanyika kwa mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing, na matokeo ya pande hizo mbili katika kukabiliana na janga la COVID-19 kwa pamoja, kufuatilia utekelezaji wa Hatua Nane zilizotolewa kwenye mkutano wa Beijing, na kupitia nyaraka mbalimbali za matokeo ya ushirikiano. Amesema, mkutano huo umeonesha nia thabiti ya pande hizo mbili kutafuta maendeleo, kukabiliana na changamoto na kunufaika na fursa kwa pamoja katika zama mpya.

Mawaziri wa mambo ya nje, mawaziri wa biashara na mawaziri wa fedha wa nchi 53 za Afrika au wawakilishi wao walihudhuria mkutano huo, na wamepongeza hatua mpya zilizotangazwa na rais Xi Jinping wa China katika kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika.