Rwanda yadhamiria kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI ifikapo mwaka 2030
2021-12-02 10:36:24| cri

Rwanda inalenga kufikia lengo la Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) la kukomesha UKIMWI ifikapo mwaka 2030. Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya wa Rwanda Bw. Daniel Ngamije wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani nchini humo.

Ameongeza kuwa matokeo ya hivi karibuni ya utafiti yanaonesha kuwa Rwanda imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na UKIMWI. Leo hii, asilimia 86 ya watu wanaoishi na UKIMWI wanafahamu hali zao, asilimia 97 ya wanaojua hali zao juu ya matibabu ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi na asilimia 90 ya wale wanaopata matibabu wamepunguza wingi wa virusi.

Aidha hii ni hatua muhimu dhidi ya lengo la UKIMWI la 90-90-90 na nchi hiyo inatarajia kufikia lengo jipya la UKIMWI la 95-95-95 lililowekwa kufikiwa katika mwaka 2030.