CGTN na vyombo vya habari vya Latin Amerika zatangaza kwa pamoja Pendekezo kuhusu hatua za vyombo vya habari
2021-12-02 22:32:28| Cri

CGTN na vyombo vya habari vya Latin Amerika zatangaza kwa pamoja Pendekezo kuhusu hatua za vyombo vya habari_fororder_微信图片_20211203092136

Wakati Mkutano wa tatu wa mawaziri wa Baraza la China-CELAC unapokaribia, leo tarehe 2 Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha China CGTN na vyombo vya habari zaidi ya 30 vya Latin Amerika zimetangaza kwa pamoja “Pendekezo kuhusu hatua za vyombo vya habari”.

Naibu mkuu wa Idara ya uenezi ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji CMG Bw. Shen Haixiong amesema katika hotuba yake kwa njia ya video kuwa, kama rais Xi Jinping alivyobainisha katika sherehe ya ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa vyombo vya habari vya China na Latin Amerika uliofanyika mwaka 2016, mawasiliano kati ya vyombo vya habari ni sehemu muhimu katika uhusiano kati ya pande hizo mbili. Bw. Shen amesisitiza kuwa CMG itaendelea kuimarisha mawasiliano na vyombo vya habari vya Latin Amerika, na kuchangia katika maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.