Tanzania yapanga kuongeza uzalishaji wa korosho
2021-12-02 10:38:06| cri

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Bodi ya korosho ya Tanzania Bw. Francis Alfred jana alisema Tanzania inapanga kuongeza uzalishaji wa korosho kwa kuwapatia wakulima miche takriban milioni 15.

Amesema miche hiyo itawapatia wakulima bila ya malipo, ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa korosho hadi tani laki 7 kwa mwaka ifikapo mwaka 2030 kutoka tani laki 3 kwa mwaka ya hivi sasa. Ameongeza kuwa kama wakulima wataongeza maeneo ya kulima, lengo la kuongeza uzalishaji linaweza kutimia, na wakulima hao watapewa mafunzo ya kilimo.