Watu zaidi ya 20 wafariki katika ajali ya meli kaskazini mwa Nigeria
2021-12-02 09:02:41| cri

Watu 20 wamefariki na wengine wengi hawajulikani walipo kufuatia ajali ya kupinduka kwa meli moja juzi jioni katika jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya jimbo la Kano inasema uchunguzi umeonesha kuwa, meli hiyo ilibeba watu kupita kiasi. Meli ilikuwa na watu wapatao 50, wengi wao wakiwa ni wanafunzi, na mizigo kadhaa.

Hadi sasa waokoaji wamewaokoa watu 7 na kupata miili 20.