IGAD yaanzisha jukwaa la kushughulikia nzige na wadudu wanaovuka mipaka
2021-12-03 08:44:54| CRI

Jumuiya ya maendeleo ya serikali za nchi za Afrika mashariki IGAD jana ilizindua jukwaa la kushughulikia nzige na wadudu wanaovuka mipaka.

IGAD imesema jukwaa hilo lina lengo la kukabiliana na nzige wa jangwani, na kuimarisha ushirikiano, usimamizi mfululizo na udhibiti wa nzige wa jangwani na wadudu wengine wanaovuka mipaka katika maeneo yanayoathiriwa.

Mkurugenzi wa kituo cha utabiri na matumizi ya hali ya hewa cha IGAD Guleid Artan ametoa wito wa juhudi za pamoja katika kushughulikia nzige wa jangwani katika kanda hiyo. Amesema udhibiti na usimamizi wenye ufanisi dhidi ya nzige wa jangwani katika eneo la IGAD na sehemu za karibu, unahitaji kushirikisha nchi zote zinazoathirika, jumuiya ya kimataifa, sekta binafsi na wadau wote wa serikali na wasio wa serikali.