Maafisa wa jeshi la Somalia na AU wanolewa ujuzi katika ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia
2021-12-06 08:31:15| cri

Wanajeshi 20 kutoka Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) wamemaliza mafunzo yao ya siku nne yanayolenga kunoa ujuzi wao katika kukusanya taarifa za kiintelijensia ambayo ni muhimu katika kudhoofisha magaidi wa al-Shabaab nchini humo.

Tume hiyo imesema Jumapili kwamba mafunzo ya kukusanya na kupeana taarifa yanalenga kuimarisha ushirikiano katika kufanya operesheni za kijeshi za pamoja dhidi ya magaidi nchini Somalia. Kamanda wa kikosi cha AMISOM Diomede Ndegeya amesisitiza umuhimu wa operesheni za kijeshi na kusema kwamba intelijensia ama taarifa ni uwezo muhimu kwenye operesheni za kijeshi, na pia ni muhimu kwa AMISOM na SNA.