China na Jamhuri ya Congo zakubaliana kuimarisha ushirikiano wao
2021-12-06 08:31:47| cri

Rais wa Jamhuri ya Congo Denis Sassou Nguesso alikutana na mjumbe wa Idara ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC anayeshughulikia sera za kigeni Bw. Yang Jiechi.

Yang amesema kutokana na umakini na uongozi wa wakuu wa nchi hizi, uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Jamhuri ya Congo umepata maendeleo makubwa, na China inapenda kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu na Jamhuri ya Congo na kuungana mikono kwenye masuala yanayohusu maslahi makuu ili kuendana na sifa na ngazi ya juu ya uhusiano kati ya nchi hizo. Amesema China itatumia fursa ya utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC kuendelea kuunga mkono Jamhuri ya Congo kupambana na janga la COVID-19, kutafuta na kupanua maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo miundombinu na sekta ya viwanda ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hizi.

Rais Sassou naye amesema nchi yake inapongeza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo na kushukuru China kwa kutoa msaada mwingi katika kupambana na COVID-19 na kuunga mkono ufufuaji wa uchumi. Amesema nchi yake inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja, kupenda kuimarisha hali ya kuaminiana na kupanua ushirikiano na China katika maeneo mbalimbali ikiwemo nishati, usafiri na kilimo.