Sudan Kusini na China zazindua awamu ya pili ya ushirikiano wa elimu
2021-12-07 09:39:37| cri

Sudan Kusini na China zimezindua awamu ya pili ya Mradi wa Ushirikiano wa Kiufundi unaosaidiwa na China ambao utawajengea uwezo walimu wa nchi hiyo na pia kuchapisha vitabu vingi vya kiada kwa ajili ya wanafunzi.

Awamu ya pili ya mradi huo utakaofadhiliwa na serikali ya China kwa kiasi cha karibu dola milioni 20 za kimarekani, pia itahusisha utayarishaji na uchapishaji wa vitabu vya shule za msingi kwa masomo ya Kiingereza, Hisabati na Sayansi, kuwajengea walimu uwezo wa kusimamia elimu.

Aidha, mpango huo pia unajumuisha uendelezaji na usambazaji wa mifumo ya tathmini ya matumizi ya vitabu vya kiada, na usambazaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na utekelezaji wa programu za lugha ya Kichina.

Makamu wa Rais wa Shirika la Huduma Bw. Hussein Abdelbagi Akol amesema awamu ya pili ya mradi huo inaonyesha uhusiano mkubwa kati ya nchi hizo mbili.