Mtaalamu wa Cameroon: Mkutano wa Dakar wa FOCAC wathibitisha mara nyingine dhamira ya China ya kuwaunga mkono ndugu wa Afrika
2021-12-07 09:29:12| CRI

Mtaalamu wa Cameroon: Mkutano wa Dakar wa FOCAC wathibitisha mara nyingine dhamira ya China ya kuwaunga mkono ndugu wa Afrika_fororder_Rodrigo

Msomi kutoka Cameroon Dkt. Taling Tene Rodrigue amesema kuanzia Mipango Kumi ya Ushirikiano iliyotolewa kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika 2015 huko Johannesburg, hadi Hatua Nane zilizowekwa mwaka 2018 kwenye mkutano wa kilele wa Beijing, hadi Miradi Tisa iliyotangazwa na Rais Xi Jinping kwenye mkutano wa Dakar, China imethibitisha kwa mara nyingine tena nia njema na dhamira yake ya kuwaunga mkono ndugu zake wa Afrika, na Waraka uitwao “Ushirikiano kati ya China na Afrika katika Zama Mpya” uliotolewa hivi karibuni na Serikali ya China, umejumuisha matunda halisi yaliyopatikana kwenye ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Dkt. Rodrigue ambaye ni naibu mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Nchi za Afrika Zinazotumia Lugha ya Kifaransa kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, pia amesema nchi nyingi za Afrika zina hamu kubwa ya kujiunga na ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kwa sababu waafrika wanaamini kuwa pendekezo hilo lililotolewa na China ni njia iliyosubiriwa kwa muda mrefu na binadamu ya kuelekea amani, ustawi, maendeleo ya kijani, mavumbuzi na ustaarabu. China na nchi za Afrika zina wajibu wa kushirikiana ili kukamilisha jukumu hilo.