Watu wasiopungua 48 wauawa kwenye mgogoro wa kikabila uliotokea eneo la Darfur, Sudan
2021-12-07 09:29:13| cri

Kamati kuu ya madaktari wa Sudan ambalo ni Shirika lisilo la kiserikali jana ilitoa taarifa ikisema, watu wasiopungua 48 wameuawa kwenye mgogoro wa kikabila uliotokea jimboni Darfur Magharibi.

Taarifa imesema ripoti ya awali imeonyesha kuwa vurugu hizo zilizotokea eneo la Kirainik jimboni Darfur Magharibi zimesababisha vifo vya watu 48, na wengine wengi wamejeruhiwa. Kwenye ripoti tofauti, Shirika jingine lisilo la kiserikali liitwalo Shirika la Uratibu wa Wakimbizi la Darfur limethibitisha kuwa waasi wamefanya shambulizi huko eneo la Kirainik jimboni Darfur Magharibi, na kusababisha vifo na majeruhi ya makumi ya watu.

Gavana wa eneo la Darfur Bw. Arko Minni Minnawi amesema wamechukua hatua mara moja ili kuzuia mfarakano wa kikabila, ambao unaweza kusababisha kuchomwa vijiji na hali ya wasiwasi zaidi.